Swali: Nikiona mtu anakula kwa kusahau naye amefunga. Nikimwambia “Acha kula au kunywa wewe umefunga!”. Je, ntakuwa mwenye dhambi? Je, nimkumbushe au nimwache mpaka atapokumbuka mwenyewe?

Jibu: Mkumbushe. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

وَالْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاء بَعْضٍ

“Na waumini wanaume na waumini wanawake wao kwa wao ni marafiki.” (09:71)

Na Mtume (swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:

“Muumini ni kio kwa muumini mwenzake.”

Anasema Allaah (Ta´ala):

وَذَكِّرْ فَإِنَّ الذِّكْرَى تَنفَعُ الْمُؤْمِنِينَ

“Na kumbusha, kwani ukumbusho huwafaa waumini.” (51:55)

Mwambie wewe umefunga, acha kula na kunywa.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://alwasabi.al3ilm.com/alfatawaa
  • Imechapishwa: 10/05/2020