Kumkopesha mtu anayetaka kufanya kazi ya haramu

Swali 13: Ni ipi hukumu ya kumkopesha mtu anayefanya kazi katika mambo ya haramu pamoja na kujua hali yake?

Jibu: Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖ وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ

“Saidianeni katika wema na kumcha Allaah na wala msisaidiane katika dhambi na uadui.”[1]

Kwa hivyo usimkopeshe na wala usimsaidie juu ya batili hii.

[1] 05:02

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tuhfat-ul-Mujiyb, uk. 63
  • Imechapishwa: 16/01/2020