Kumkopa pesa muislamu mtenda madhambi


Swali: Kuna mtu aliniomba nimkope kiwango cha pesa pamoja na kuwa ni mvuta sigara. Je, nimkopeshe au hapana?

Jibu: Midhali ni muislamu basi inafaa kwako kumkopa na kumpa swadaqah. Imekuja katika Hadiyth:

“Ambaye atamkopesha mtu mara mbili basi mara moja inakuwa swadaqah.”

Huenda kule kumkopesha kwako ikawa ni sababu ya kukubali nasaha na kuwa karibu na wewe. Kwa hivyo tumia fursa ya kumpa nasaha na kumtendea wema. Mtu akiwa ni fakiri au mtenda madhambi kama kuvuta sigara mpe chakula akiwa ni mwenye njaa, mpe swadaqah na mnasihi. Huyu vivyo hivyo mkope na umnasihi vilevile.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (02) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/429/429.mp3
  • Imechapishwa: 11/03/2018