Kumkodishia nyumba na duka anayetaka kufanya maasi

Swali: Ni ipi hukumu ya kukodisha maduka ya biashara kwa anayefungua saluni ya kunyoa, kushona kwa wanawake, uuzaji wa kanda za video au kanda za nyimbo?

Jibu: Haifai kumkodishia duka ambaye analitumia kumuasi Allaah. Duka linakodishwa kwa anayelitumia katika mambo ya halali. Anayemkodishia anayenyoa ndevu za watu, zana za pumbao, anauza pombe au vyenginevyo katika maasi hakodishiwi. Haijuzu popote pale. Haijalishi kitu hata kama ni Marekani na kwenginepo. Muda wa kuwa ni muislamu basi haifai kwake kusaidia juu ya kumwasi Allaah. Ni mamoja kwa kukodisha au kwa njia nyingine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/3632/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%AA%D8%A7%D8%AC%D9%8A%D8%B1-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%AD%D9%84%D8%A7%D8%AA-%D9%84%D8%A7%D9%85%D9%88%D8%B1-%D9%85%D9%86%D9%83%D8%B1%D8%A9-%D8%A7%D9%88-%D9%85%D8%B4%D8%A8%D9%88%D9%87%D8%A9
  • Imechapishwa: 28/02/2020