Kumkodishia nyumba mtenda madhambi


Swali: Je, inafaa kuwakodishia maduka watenda maasi akiwemo mnyoa ndevu na mwenye kuacha swalah?

Jibu: Haifai kuwakodishia makafiri. Miongoni mwao ni manaswara, wanaotambulika kwa shirki kama vile mabudha na mfano wao. Kuhusu muislamu mtenda dhambi inafaa kumkodishia. Lakini ukiwapata wema ndio bora. Kuhusu kumkodishia ambaye atafanya maasi ndani yake, kwa mfano ambaye atafanya kazi yake humo ni saluni ya kuwanyoa watu ndevu, kazi za ribaa, kuuza pombe na madawa ya kulevya, ni jambo lisilofaa. Kwa sababu kufanya hivo ni kuwasaidia juu ya dhambi na uadui.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa-ud-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/4843/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%AA%D8%A7%D8%AC%D9%8A%D8%B1-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%AD%D9%84%D8%A7%D8%AA-%D9%84%D8%A7%D8%B5%D8%AD%D8%A7%D8%A8-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B9%D8%A7%D8%B5%D9%8A
  • Imechapishwa: 22/11/2020