Kumkataa Mchumba Mwenye Dini Kwa Kutarajia Mwengine Aliye Bora Zaidi


Swali: Inajuzu kwangu kumkatalia kijana mwenye kuhifadhi swalah na mwenye dini ambaye amekuja kunichumbia lakini hata hivyo natafuta kijana mwengine ambaye ni mkamilifu zaidi katika dini na akili kuliko kijana huyu?

Jibu: Haijuzu kwa mtu kuiacha fursa pale anapoipata. Pindi mtu anapopata mtu mwenye tabia na dini nzuri asimwache kwa ajili ya kutafuta mwengine ambaye ni mbora zaidi. Hili ni kwa sababu unayotaka heunda usiyapate khaswa pale ambapo mwanamke anakuwa ameshakuwa mkubwa. Katika hali hii haifai kwake kabisa kumpuuza yule aliyemchumbia. Mtume (Swalla Allaahu ?alayhi wa sallam) amesema:

“Atapokujieni yule ambaye mnaridhia kwake dini na tabia yake muozeni.”

Aolewe ikiwa mchumba huyo? kunaridhiwa kwake dini na tabia yake. Asisubirie kitu ambacho hajui huenda kikatokea kweli au kisitokee.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (12)
  • Imechapishwa: 27/05/2017