Kumjuza mteja kwamba kuna bidhaa ya bei nafuu kidogo


Swali: Mimi nafanya kazi kwenye duka la madawa. Wakati anapokuja mteja na kuniomba dawa fulani ni lazima kwangu kumjuza kwamba zipo dawa mfano wake ambazo ni bei nafuu kuliko hiyo aliyoomba?

Jibu: Mpe hiyo aliyoomba. Kama yuko na cheti kutoka kwa daktari basi mpe dawa hiyo. Lakini akiwa hana cheti kutoka kwa daktari basi usimpe. Kwa sababu pengine ikamdhuru pasi na yeye kujua.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.alfawzan.af.org.sa/ar/node/18365
  • Imechapishwa: 11/06/2021