Kumhijia asiyeweza kuhiji pasina idhini yake

Swali: Ni ipi hukumu ya kumfanyia Hajj au ´Umrah pasina idhini ya anayefanyiwa hivo ikiwa ni katika wale ambao hawawezi kufanya Hajj?

Jibu: Ni lazima kupatikane idhini yake. Kwa kuwa huku ni kuwakilisha. Ni lazima kupatikane idhini ya muwakilishaji ili aweze kunuia. Kwa kuwa kila ´Ibaadah ni lazima kupatikane nia. Sababu ni ili yule muwakilishaji aweze kunuia anayemhijia. Ama maiti hakuhitajii idhini kwa kuwa hawezi kutoa idhini. Afanyiwe Hajj. Ama aliye hai, ni lazima ichukuliwe rai yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (23) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-04-12.mp3
  • Imechapishwa: 14/11/2014