Kumgusa mwanamke nyuma ya kizuizi kunachengua wudhuu´?

Swali: Je, kumgusa mwanamke nyuma ya kizuizi kwa matamanio kunachengua wudhuu´?

Jibu: Maoni ya sawa ni kwamba hakuchengui wudhuu´. Ni mamoja moja kwa moja au nyuma ya kizuizi. Isipokuwa ikiwa kama atatokwa na kitu. Akitokwa na kitu, kama madhiy, basi hapo wudhuu´ wake unachenguka. Asipotokwa na kitu hakuna neno. Amesema (Ta´ala):

أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ

“… au mmewagusa wanawake… “[1]

Kinachokusudiwa hapa ni kumwingilia. Masuala haya wanachuoni wana rai tatu:

1- Maoni ya kwanza wapo waliosema kwamba kumgusa mwanamke kunachengua wudhuu´ moja kwa moja. Ni mamoja mtu amefanya hivo kwa matamanio au pasi na matamanio. Haya ndio maoni ya ash-Shaafi´iy. Anaona kwamba mkono wako ukigusa mkono wa mwanamke basi unatakiwa kutawadha tena. Wanaona pia kwamba mtu akiwa anatufu kwenye Ka´bah basi ajitahidi mkono wake usiguse mkono wa mwanamke mwingine. Hili ni gumu sana khaswa kutokana na msongamano wa wakati huu?

2- Maoni ya pili yanasema kuwa wudhuu´ unachenguka akimgusa mwanamke kwa matamanio na akimgusa pasi na matamanio hauchenguki.

3-  Maoni ya tatu wanaona kuwa wudhuu´ hauchenguki kabisa. Ni mamoja amemgusa mwanamke kwa matamanio au pasi na matamanio. Isipokuwa akitokwa na kitu. Haya ndio maoni ya sawa. Dalili juu ya hili ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akibusu ilihali amefunga na wakati mwingine anabusu na anaenda kuswali na wala hatawadhi tena.

[1] 04:43

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (06) http://dl.islamweb.net/audiopath/audio/lecturs/aalrrajhee/433/433.mp3
  • Imechapishwa: 07/12/2018


Takwimu
  • 27
  • 413
  • 1,821,446