Swali: Ikiwa mtu ametawadha au yuko katika Wudhuu, akamgusa mama yake au dada yake. Je, Wudhuu wake unavunjika?

Jibu: Kauli sahihi ni kwamba, kumgusa mwanamke hakuvunji Wudhuu, sawa ikiwa ni mke wake au wanawake wengine. Hii ndio kauli sahihi. Na kuna tofauti kwa wanachuoni. Wanachuoni kuhusiana na hili wana kauli tatu;

1) kumgusa mwanamke kunavunja Wudhuu kabisa,

2) hakuvunji Wudhuu kabisa na

3) kuna ufafanuzi, kunavunja Wudhuu ikiwa amemgusa kwa matamanio, vinginevyo hapana.

Na kauli yenye nguvu katika kauli hizi tatu ni kwamba, (kumgusa mwanamke) hakuvunji Wudhuu kabisa. Kutokana na yaliyothibiti kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa aliwabusu baadhi ya wake zake kisha akaswali na wala hakutawadha. Na ni kwa sababu, asli ni kuwa mtu anabaki na Twahara na wala haivunjiki isipokuwa kwa kitu cha wazi. Na ni kwa sababu jambo hili wanakumbana nalo sana katika manyumba yao, na lau kumgusa mwanamke kungekuwa kunavunja Wudhuu angelibainisha hilo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ubainisho wa wazi na asingelificha. Ama Kauli Yake (´Azza wa Jalla):

أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ

“Au mmewagusa (mmewaingilia) wanawake.” (04:43)

Makusudio ya hilo ni Zinaa, kama alivyosema hilo Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) na wengineo. Makusudio ni jimaa, Allaah Kaiita kwa jina na kugusa. Allaah Kaipa jimaa kunya kwa lafdhi kama hii na kwa “kukutana”. Hii ndio kauli sahihi, ya kuwa kumgusa mwanamke hakuvunji Wudhuu isipokuwa tu mtu akitokwa na kitu, kama madhiy. Vinginevyo hakutengui Wudhuu. Swali:Huku kwetu watu wanawasomea Qur-aan maiti na wanachukua ujira kwa hilo. Anapokufa mmoja wao wanamsomea Qur-aan kwa siku tatu, wanamchinjia na kumfanyia walima. Je, maiti wanafaidika kwa lolote na je hili ni katika Shari´ah?

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb
  • Imechapishwa: 25/03/2018