Swali: Mtawala akihukumu kinyume na yale aliyoteremsha Allaah afanyiwe uasi kwa sababu ametenda kufuru?

Jibu: Asimfanyie uasi isipokuwa kama alivyosema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“… isipokuwa mpaka pale mtakapoona kufuru ya wazi kabisa ambayo mna dalili kwayo kutoka kwa Allaah.”

Ni lazima kupatikane mambo haya mane:

La kwanza: Kufuru.

La pili: Ya wazi kabisa.

La tatu: Mna dalili kwayo kutoka kwa Allaah.

Ikiwa ni kufuru ambayo watu wana mashaka nayo haifai [kumfanyia uasi]. Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“… ya wazi kabisa.”

bi maana haina utata. Iwe mna dalili kwayo kutoka kwa Allaah.

Jengine ni kwamba kumeshurutishwa masharti mawili juu ya kumfanyia uasi:

La kwanza: Kupatikane dalili. Nchi ikiwa ni ya kikafiri na mtawala ni kafiri, isimikwe nchi ya Kiislamu na mtawala muislamu. Ama kumg´oa mtawala kafiri na kuleta kafiri mwengine, lengo halikufikiwa. Kukiondoshwa mtawala kafiri basi ni lazima aletwe mtawala muislamu ambaye atasimamisha Shari´ah ya Allaah katika ardhi.

La pili: Uwezo wa kufanya hivo. Lakini ikiwa hawawezi – hata kama nchi itakuwa ya kikafiri na mtawala akawa kafiri – ni kipi wanachoweza kufanya? Wakijaribu wanauawa na mambo yanakoma.

Kwa hivyo ni lazima kuwepo uwezo na kupatikane dalili pamoja vilevile na kupatikane masharti; kufuru yake iwe ya wazi kabisa na muwe na dalili kutoka kwa Allaah. Inahusiana na kufuru ya wazi kabisa isiyokuwa ndani yake na mashaka. Vinginevyo wanachotakiwa ni watu kuwa na subira – hata kama nchi ya kikafiri na mtawala ni kafiri – mpala pale Allaah atapowasahilishia waislamu jambo lao.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (03) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/430/430.mp3
  • Imechapishwa: 03/04/2018