Kumfunua maiti uso baada ya kumtia ndani ya kaburi

Swali: Katika mji wetu watu wamezowea kumfunua maiti uso baada ya kumtia ndani ya kaburi. Je, tendo hili ni katika Sunnah au hapana?

Jibu: Hili sio katika Sunnah. Hili ni katika matendo ya wajinga. Hakufunuliwi kitu kwa maiti. Akivikwa sanda hafunuliwi kitu chochote kutoka kwake. Isipokuwa kwa yule anayetaka kumbusu, hakuna neno. Lakini baada ya hapo afike anamfunika.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Sharh Zaad-il-Ma´aad (10) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1430-10-29.mp3
  • Marejeo: Firqatunnajia.com
  • Imechapishwa: 11/11/2014