Kumfuata imamu kwenye TV au redio


Swali: Je, mswaliji anaweza kuwafuata waswaliji kwenye TV au haijuzu kufanya hivo?

Jibu: Hapana, asiwafuate. Isipokuwa akiwa msikitini ambapo anasikia sauti ya imamu. Ama akiwa nyumbani kwake au kwenye maduka mengine asiwafuate. Bali ni wajibu kwake ajitahidi kwenda msikitini na aswali pamoja na wengine. Ama akiwa nyumbani kwake au sehemu nyingine aswali peke yake. Asimfuate imamu.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alifta.net/Fatawa/fatawaChapters.aspx?languagename=ar&View=Page&PageID=1232&PageNo=1&BookID=5
  • Imechapishwa: 20/03/2018