Kumfanyia ´Umrah ndugu aliyepatwa na kansa

Swali: Mmoja katika ndugu zangu amepatwa na maradhi sugu ambayo ni kansa ya kwenye ubongo. Je, inafaa kwangu kumfanyia ´Umrah kwa kuzingatia kwamba hawezi kutikisika?

Jibu: Ikiwa hakuwahi kufanya ´Umrah hapo mwanzoni, hakuna neno. Ama kama aliwahi kufanya ´Umrah hapo kabla asifanyiwe.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (20) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Umdah-6-2-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 03/01/2020