Kumfanyia mgonjwa matabano kwa zafarani

Swali: Ni ipi hukumu ya matabano ambayo huandikwa kwenye karatasi au sahani kwa rangi ya zafarani kisha inaoshwa na kunywewa?

Jibu: Ikiwa sio talasimu basi nataraji kuwa hakuna neno. Ibn-ul-Qayyim ametaja kwamba yamefanywa na baadhi ya wanafunzi wa Imaam Ahmad. Lakini imeshurutishwa watu wasiendi mbali zaidi. Kule kujipaka kichwa chake rangi ya zafarani au mfano wa kitendo kama hicho hakitakiwi. Msingi ni kusomewa mgonjwa na kufanyiwa matabano au kukasomwa ndani ya maji kisha akayaoga au akayanywa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (17)
  • Imechapishwa: 13/11/2020