Swali: Je, tunaweza kuwachukulia manaswara kuwa ni ndugu zetu kama tunavyofanya kwa waislamu bila ya kutenganisha?

Jibu: Ni haramu kuwafanya manaswara kuwa ni ndugu. Amesema (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَىٰ أَوْلِيَاءَ ۘ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ

“Enyi mlioamini! Msiwafanye mayahudi na manaswara kuwa ni marafiki – wao kwa wao ni marafiki. Na yeyote katika nyinyi atakayefanya urafiki nao, basi hakika yeye ni miongoni mwao. Hakika Allaah haongoi watu madhalimu.” (05:51)

إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ

“Hakika si vyenginevyo waumini ni ndugu.” (49:10)

Allaah amefanya udugu wa kikweli uko kati ya waumini. Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba amesema:

“Muislamu ni ndugu ya muislamu mwenzake.”

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (2/46)
  • Imechapishwa: 24/08/2020