Swali: Mwenye kuwachukia baadhi ya Maswahabah kutokana na walioyafanya kabla ya kuingia katika Uislamu, kwa mfano yule aliyemuua Hamzah, kwa hali kama hii itahesabika anawachukia Maswahabah?

Jibu: Hili halina shaka. Hili halina shaka. Huyu anaonelea kuwa Uislamu na Tawbah haifuti madhambi yaliyotangulia – na tunaomba kinga kwa Allaah. Allaah (´Azza wa Jall) Amesema:

قُل لِّلَّذِينَ كَفَرُوا إِن يَنتَهُوا يُغْفَرْ لَهُم مَّا قَدْ سَلَفَ

“Sema [uwaambie] waliokufuru [kwamba]: wakikoma wataghufuriwa yaliyopita.” (08:38)

Wamesamehewa. Pindi walipotubu na kusilimu Allaah Aliwasamehe. Mwenye kutubu kwa dhambi ni kama ambaye hana dhambi. Huyu anapekua makosa ya Maswahabah na kutaka propaganda ya kuingiza maneno kama haya ya kipotevu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (13) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_13.mp3
  • Imechapishwa: 20/06/2018