Swali: Imethibiti katika Hadiyth ya kwamba yule atayejenga uadui na walii wa Allaah basi amejenga uadui na Allaah. Inamgusa yule mwenye kujenga uadui na walii wa Allaah kwa sababu za kibinafsi na sio kwa kufuata yale Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) waliyoamrisha?

Jibu: Akimjengea uadui kwa sababu za kibinafsi ni kufuata matamanio. Sio kuchukia kwa ajili ya Allaah. Itakuwa ni kuchukia kwa ajili ya kufuata matamanio. Hii ni dhambi kubwa. Huyu ameyafanya matamanio yake kuwa mungu. Anapenda kwa ajili ya matamanio yake na anachukia kwa ajili ya matamanio yake. Anatoa kwa ajili ya matamanio yake na anazuia kwa ajili ya matamanio yake. Huyu ameyafanya matamanio yake kuwa mungu wake. Hii ni khatari kubwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (03) http://alfawzan.af.org.sa/node/2046
  • Imechapishwa: 20/10/2016