Kumchelewesha maiti kidogo kwa sababu ya uchunguzi

Swali: Je, Sunnah ni kuharakisa jeneza au kuchelewesha ili watu wakusanyike?

Jibu: Sunnah ni kuharakisha isipokuwa pakiwa sababu. Wanachuoni wamesema kuwa imependekezwa kuharakisha. Imekuja katika Hadiyth:

“Haitakikani maiti ya muumini kubakizwa juu ya migongo ya famili yake.”

Wanachuoni wamesema kwamba isipokuwa tu akifa ghafla. Basi katika hali hiyo atacheleweshwa mpaka ihakikishwe sababu ya kifo chake, jambo ambalo hufanyika katika mahospitali ya sasa. Kupitia ucheleweshwaji mdogo usiodhuru ambao kwa ajili yake watu wamekusanyika kwa ajili ya kuja kutoa pole itapata kutambulika sababu ya kifo chake. Hapo ni pale ambapo wakati utakuwa sio mrefu. Ama kumchelewesha kwa muda mrefu ni jambo lisilotakiwa.

Haitakikani kuchelewesha jeneza lake. Lakini kwa mfano akicheleweshwa kuanzia alfajiri mpaka adhuhuri, kuanzia adhuhuri mpaka alasiri, ni sawa. Ama kumchelewesha kwa siku moja au mbili ni jambo lisilotakiwa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (11) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191491#219817
  • Imechapishwa: 28/06/2019