Kumbusu mke mchana wa Ramadhaan


Swali: Mwanamume akimbusu mke wake mchana wa Ramadhaan au akacheza naye swawm yake inaharibika?

Jibu: Mwanamume kumbusu mke wake, kucheza naye au kumpapasa pasi na kufanya naye jimaa yote hayo yanajuzu na wala hayana ubaya. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akibusu na kupapasa ilihali amefunga. Lakini akichelea kutumbukia katika yale aliyoharamisha Allaah kwa sababu matamanio yake ni yenye kuja kwa haraka basi itakuwa inachukiza kwake kufanya hivo. Akitokwa na manii basi ni lazima kwake kujizuia na kula na kunywa na halazimiki kutoa kafara kwa mtazamo wa wanachuoni wengi. Kuhusu madhiy hayaharibu swawm kwa mujibu wa maoni yaliyo sahihi zaidi ya wanachuoni. Kimsingi ni usalama na kutokubatilika swawm. Jengine ni kwa sababu ni vigumu pia na kujiepusha nayo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/315)
  • Imechapishwa: 02/06/2018