Kumbusu mke baada ya kutawadha kunachengua wudhuu´?

Swali: Ni ipi hukumu kwa mwenye kumbusu mke wake akiwa na twahara na anataka kuswali?

Jibu: Hakuna neno juu yake. Akimbusu mke wake na asitokwe na kitu wudhuu´ wake ni sahihi kutokana na maoni yenye nguvu. Wako wanachuoni wenye kuona kuwa kumbusu kunachengua wudhuu´. Wengine wakasema kile kitendo cha kumgusa tu kunachengua wudhuu´. Maoni ya sawa ni kwamba hayachengui wudhuu´. Haya ndio maoni yenye nguvu katika maoni ya wanachuoni kwamba kumgusa mwanamke au kumbusu hakuchengui wudhuu´ kwa sharti asitokwe na kitu; si madhiy wala kitu kingine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdil-´Aziyz bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3788/هل-تقبيل-الزوجة-ينقض-الوضوء
  • Imechapishwa: 05/04/2020