Swali: Je, inajuzu kumbusu maiti kabla ya kumzika?

Jibu: Hakuna neno. Imethibiti kwamba wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipofariki Abu Bakr (Radhiya Allaahu ´anh) alikuja akamfunua Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akambusu:

“Uko mzuri ulipokuwa hai na katika hali ya kufa.”

Kifo ambacho Allaah amekuandikia kimekwisha. Abu Bakr as-Swiddiyq, ambaye ndiye mbora wa Ummah baada ya Mtume wake, alimbusu Mtume baada ya kifo chake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://shrajhi.com.sa/fatawa/64/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%AA%D9%82%D8%A8%D9%8A%D9%84-%D8%A7%D9%84%D9%85%D9%8A%D8%AA
  • Imechapishwa: 20/12/2019