Kullaabiyyah na Ashaa´irah wanakaribiana juu ya maneno ya Allaah

Kuna wenye kuona kuwa hakuna tofauti kati ya madhehebu ya Kullaabiyyah na Ashaa´irah. Baadhi ya Ashaa´irah wanaonelea kuwa ni madhehebu moja tu. Kwa sababu madhehebu yote mawili yamekubaliana juu ya kwamba maneno ni maana iliosimama katika nafsi yake Allaah na kwamba herufi na sauti zinatolea dalili kuonesha Maneno ya Allaah. Kulaabiyyah wamesema maneno ya Allaah ni hikaya na Ashaa´irah wamesema kuwa ni ibara. Hivyo madhehebu ya Ashaa´irah na Kullaabiyyah yakawa ni madhehebu yenye kukaribiana. Madhehebu ya Ashaa´irah watu wake wanadai kuwa ni Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/166-167)
  • Imechapishwa: 30/05/2020