Kulisindikiza jeneza kwa mbele au kwa nyuma?

Swali: Kulisindikiza jeneza kunakuwa kwa mbele yake ikiwa ni kwa kutembea na nyuma yake ikiwa ni kwa kupanda juu ya kipando?

Jibu: Wanachuoni wametofautiana juu ya haya. Sahihi ni kwamba hakuna neno kwa yule mwenye kutembea mbele au nyuma yake. Muhimu ni kwamba aliandame mpaka azikwe.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (01) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=190884#219018
  • Imechapishwa: 03/01/2018