Kulipa swawm ya sunnah ambayo alipata hedhi


Swali: Kuna mwanamke anafunga swawm ya Sunnah ya Alkhamisi na Jumatatu. Ipo siku ambapo alipata hedhi kabla ya jua kuzama. Je, ailipe siku hiyo?

Jibu: Swawm ya Sunnah hailipwi. Swawm ya faradhi ndio yenye kulipwa. Ama swawm ya Sunnah hailipwi. Hata hivyo akitaka kufunga siku nyingine badala ya siku hii kwa minajili ya kutaka kufanya matendo mema zaidi, na sio kwa minajili ya kuilipa, anapata kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (12) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-08-02.mp3
  • Imechapishwa: 03/06/2018