Kulipa swalah ya safarini unapofika katika mji wako


Swali: Nikiwa katika safari ambayo mtu anaweza kufupisha Swalah, na Swalah ya ´Aswr ikanifikia na sikuiswali mpaka wakati wake ulipokwisha na nikafika kwa ahli zangu. Je, nilipe Swalah ile kwa kufupisha au kikamilifu?

Jibu: Msafiri akifika kwa ahli zake, analipa (Swalah) zilizompita kikamilifu na hafupishi. Anafupisha tu katika hali yake ya safari, ama akichelewesha kwa mfano ´Aswr, au Dhuhr au ´Ishaa mpaka akafika kwa ahli zake, ataswali Rakaa´ nne, kwa kuwa rukhusa alikuwa nayo katika hali ya safari.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb
  • Imechapishwa: 25/03/2018