Swali: Inajuzu kulipa deni langu la siku moja kabla ya Ramadhaan siku ya jumatano inayokuja?

Jibu: Kwanza tunasema yule ambaye yuko na deni la Ramadhaan basi aanze kulipa kuanzia kesho jumatatu. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza mtu kufunga siku moja au mbili kabla ya Ramadhaan. Lakini ikiwa haikuwezekana – mwanamke anaweza kuwa na hedhi inayomzuia kufunga – ni sawa akafunga jumatano au alkhamisi ikiwa sio katika Ramadhaan.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (41) http://binothaimeen.net/content/1495
  • Imechapishwa: 14/05/2018