Swali: Mwanamke anataka kulipa deni lake la Ramadhaan siku nane. Je, inahesabiwa akifunga siku ya ´Aashuuraa’?

Jibu: Inategemea na nia yake. Kila kitendo kinategemea na nia. Akinuia kulipa deni lake, ihesabika kuwa ni deni peke yake. Akinuia kufunga siku ya ´Aashuuraa’, itahesabika kuwa ni siku hiyo. Haziingiliani.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (17) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdtf-08011435.mp3
  • Imechapishwa: 02/11/2019