Kulipa Deni Kwa Pesa Nyingine 2


Swali: Nilikopa kutoka kwa rafiki yangu pesa za dola. Inajuzu kulipa pesa hizi kwa pesa zingine zilizo sawasawa kama mfano wa za kiyemeni au za kimisri?

Jibu: Ndio. Hakuna neno kukopa pesa na kulipa kwa pesa zingine maadamu yule mkopeshaji yuko radhi. Imethibiti ya kwamba Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

“Nilikuwa nikiuza ngamia makaburini. Nilikuwa nikiziuza kwa pesa za vipande vya dhahabu na nikipokea kwa pesa za vipande vya fedha, nikiuza kwa pesa za vipande vya fedha na nikipokea kwa kwa pesa za vipande vya dhahabu; nikichukua kimoja kwa kingine na nikipokea kimoja kwa kingine. Nikaenda kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye alikuwa nyumbani kwa Hafswah na kumwambia: “Nauza kwa pesa za vipande vya dhahabu na nikipokea kwa pesa za vipande vya fedha; nikichukua kimoja kwa kingine na nikipokea kimoja kwa kingine.” Akasema: “Hakuna neno kuchukua kwa thamani ya siku hiyo midhali hamjatengana ilihali hakujachukuliwa chochote.”[1]

Ukikopa dola na ukamlipa mwenye deni lile pesa za kisaudi, kiyemeni, kijordani au za kiiraki, na pesa ikawa kupeana mkono kwa mkono, hakuna neno. Unaweza vilevile kumlipa zaidi kwa kuwa amekutendea wema. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Watu bora ni wale wenye kulipa deni kwa [njia] bora.”

Inafaa vilevile iwapo kwa mfano atakuuzia gari kwa 10.000$ uliyonunua kwa kiwango sawasawa na pesa za vipande vya dhahabu, pesa za kisaudi, pesa za kiyemeni na mfano wake. Kwa sharti upeanaji pesa uwe mkono kwa mkono wakati wa kukutana, na kwamba msitengane bila ya chochote kutochukuliwa na umlipe thamani ilio na bidhaa hiyo sokoni siku hiyo.

[1] Abu Daawuud (3554).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.binbaz.org.sa/noor/4116
  • Imechapishwa: 01/04/2017