Kulipa ambayo mtu aliacha baada ya kubaleghe


Swali: Mimi ni msichana niliye na miaka kumi na nne ambaye nilipata ada ya mwezi ambapo nikasikia haya kumweleza mama yangu. Baada ya Ramadhaan sikulipa pamoja na kuzingatia kwamba hayo yalitokea miaka kumi na moja kabla. Ni ipi hukumu ya hilo? Hivi sasa nishaolewa.

Jibu: Ni wajibu kwako kulipa masiku yote ambayo hakufunga baada ya kujiwa na ada ya mwezi pamoja na kutubia vilevile, kuomba msamaha na kulisha masikini 1,5 kg kwa kila siku moja kwa chakula kilichozoeleka katika mji.  Wape baadhi ya mafukara. Kwa sababu mwanamke anapopata hedhi ´ibaadah zinakuwa ni zenye kumuwajibikia hata kama hajafikisha miaka kumi na tano.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/186-187)
  • Imechapishwa: 18/05/2018