Kulingania watu kwa kumithili Moto na Pepo


Swali: Umezungumzia masuala ya picha. Je, inajuzu kuchukua baadhi ya picha kuhusu siku ya Qiyaamah…

Jibu: Hapana. Hapana. Hili ni jambo linafanywa na baadhi ya vijana kwa minajili ya kulingania katika dini ya Allaah kama wanavodai. Wanapiga picha moto, pepo, miti na kadhalika. Jambo hili halijuzu. Hii ni katika elimu ya ghaibu ambayo hakuna yeyote anayeijua isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Haijuzu upuuzi kama huu.

Kulingania katika dini ya Allaah haiwi kwa mfumo kama huu. Kulingania katika dini ya Allaah inakuwa kwa Qur-aan na Sunnah. Kuvutia na kukhofisha na kubainisha. Wanachimba kaburi na kusema kuwa kufanya hivi ni kwa ajili ya kulingania katika dini ya Allaah na kukumbusha. Kumbusha watu kwa kutumia Qur-aan:

فَذَكِّرْ بِالْقُرْآنِ مَن يَخَافُ وَعِيدِ

“Basi mkumbushe kwa Qur-aan anayekhofu onyo Langu.” (50:45)

Yule asiyewaidhika kwa Qur-aan hawezi kuwaidhika kwa kumchimbia shimo. Huku ni katika kujikalifisha ambako Allaah Hakuteremsha dalili yoyote juu yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mntq--14340427.mp3
  • Imechapishwa: 19/09/2020