Kulingana kwa Allaah maana yake ni kutawala?


Swali: Vipi tutamraddi yule mwenye kusema kwamba kulingana juu ya ´Arshi maana yake ni kutawala? Wao wanasema ni vipi Allaah atalingana juu ya kitu ambacho Yeye ni mkubwa kuliko kitu hicho.

Jibu: Swali hili limetokana na kutafiti namna. Tusema hatutafui namna ya kulingana. Amelingana vile kunakolingana na utukufu na ukubwa wake. Kufasiri kwamba maana yake ni kutawala ni tafsiri batili kama walivyobainisha wanachuoni kwa njia nyingi. Hizi ni miongoni mwa tafsiri za watu wa batili na ni miongoni vilevile mwa utatizi wao batili. Haya ni kwa sababu wamefananiza kulingana kwa Allaah na kulingana na viumbe. Tunamuomba Allaah usalama na afya.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (03) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/430/430.mp3
  • Imechapishwa: 13/03/2018