Swali: Je, imethibiti kutoka kwa yeyote katika Salaf kwamba amefasiri Allaah kulingana (استواء) juu ya ´Arshi kuwa amekaa?

Jibu: Maana ya kulingana katika lugha inayotambulika, ni kama alivosema Imaam Maalik:

“Kulingana kunatambulika.”

Wanazuoni wametaja kwamba kulingana kuna maana nne:

1 – Kutulia na kuthibiti (استقر).

2 – Kuwa juu (علا).

3 – Kupanda (صعد).

4 – Kuwa juu (ارتفع).

 Kuhusu ni namna gani Mola amelingana hakuna anayejua namna yake isipokuwa Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (23)
  • Imechapishwa: 20/11/2021