Kuleta watoto wanaoleta vurugu msikitini wakati wa darsa

Swali: Hatuwezi kusikia vizuri kwa sababu ya msongamano wa watoto. Kuna ndugu mmoja amenambia kwamba mkutano uliopita watoto walikuwa wanafika ishirini.

Jibu: Ikiwa watoto wanawashawishi waliohudhuria, basi haijuzu kwake wasimamizi wao kuwaleta misikitini. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimkataza mwenye kula vitungu saumu kuukaribia msikiti na akatoa sababu ya hilo kwa kusema:

“Malaika wanaudhika kwa yale wanayoudhika kwayo watu.”

 Kila kinachowaudhi waswaliji basi haijuzu kukileta.

Kumebaki kitu kimoja; nacho ni kwamba baadhi ya watu wanalalamika juu ya kifaa cha Bayaajir[1]. Baadhi ya watu wanakipaza sauti yake na wakati mwingine kinacheza ilihali wako katika Sujuud ambapo hawezi kukinyamazisha, kunatokea kwa ajili hiyo tashwishi. Tunasema yule aliye na Bayaajir azinduke. Ina vifungo ambavyo mtu anaweza kuizima wakati anapokuja kuswali ili watu waweze kusalimika na shari yake.

[1] Tazama https://en.wikipedia.org/wiki/Pager

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (37) http://binothaimeen.net/content/841
  • Imechapishwa: 08/04/2018