Swali: Nini anachosema mwenye kuswali baada ya kumaliza kuswali Tarawiyh na kutoa salamu?

Jibu: Kuhusu anapomaliza Tarawiyh kwa kumalizia na Witr, pale anapomaliza Witr na kutoa salamu aseme “Subhaanak al-Malik al-Qudduus” mara tatu na na mara ya tatu anyanyue sauti yake.

Ikiwa ni kisimamo cha usiku bila ya Witr, sijui kama kuna kitu juu ya hili kwa kuwa hii sio kama swalah tano ambapo mtu akimaliza anasema “Astaghfiru Allaah” mara tatu na kusema “Allaahumma antas-Salaam, wa minkas-salamu… ”. Vilevile sijui kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisema kitu baada ya kumaliza Swalah za Sunnah, sawa katika Swalah ya Raatibah na Qiyaam-ul-Layl. Isipokuwa alipokuwa akimaliza Witr ndio alikuwa akisema “Subhaanak al-Malik al-Qudduus” na mara ya tatu ananyanyua sauti yake kama ilivyokuja katika Hadiyth.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kanda “Liqaa´aatu Ramadhwaaniyyah”, sehemu ya 01
  • Imechapishwa: 23/09/2020