Swali: Mtu akitenzwa nguvu kumpa mkono mwanamke mzee afanye hivo kwa ajili ya kumsalimia kwa kuwa hii ndio ada ya mji wetu?
Jibu: Hapana. Mwanamke ambaye sio Mahram hapewi mkono, sawa ikiwa ni mzee au si mzee. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anawapa bay´ah wanawake kwa maneno na mkono wake haukuwahi kugusa mkono wa mwanamke ambaye sio halali kwake. Alikuwa anawapa bay´ah wanawake kwa maneno tu.
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (33) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1431-10-24_0.mp3
- Imechapishwa: 15/11/2014