Kunyamaza Sunnah wakati wa kula?


Swali: Je, ni adabu kunyamaza wakati wa kula?

Jibu: Hakuna msingi juu ya hilo. Msingi wakati wa kula na mambo mengine yote ni:

“Yule anayemuamini Allaah na siku ya Mwisho aseme yaliyo na kheri au anyamaze.”

Mambo yanatakiwa kuwa hivyo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Raabigh (3)
  • Imechapishwa: 22/07/2017