Kula na kunywa wakati wa swawm ya sunnah

Swali: Ni ipi hukumu ya kula na kunywa katika swawm iliyopendekezwa?

Jibu: Kula na kunywa kipindi cha funga yote mawili yanaharibu funga. Kama funga hiyo ni ya lazima basi anapata dhambi. Na kama funga hiyo ni ya kujitolea basi hakuna ubaya akaivunja, kwa sababu ni swawm ya kujitolea. ´Ibaadah zote zilizopendekezwa inafaa kuzivunja, isipokuwa tu ´ibaadah ya Hajj na ´Umrah. Hajj na ´Umrah ni lazima kuzikamilisha hata kama ni ´ibaadah za kujitolea tu. Lakini imechukizwa kwa mtu kuvunja ´ibaadah zilizopendekezwa bila ya sababu sahihi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/275)
  • Imechapishwa: 10/05/2021