Kula kwa mkono wa kushoto ili mtu asichafue kikombe

Swali: Wakati mwingine wakati wa kula kunakuwepo baadhi ya vinywaji au maji na hivyo inakuwa kuna uzito kwa mtu kutumia mkono wa kulia ili chombo kisichafuke. Je, inajuzu kwake kunywa kwa mkono wa kushoto katika hali hii?

Jibu: Hapana, haijuzu kunywa kwa mkono wa kushoto katika hali hii.

Isitoshe matabibu wanakataza kunywa baada tu ya kumaliza kula. Wanasema angalau kwa uchache basi anywe baada ya nusu saa na asinywe na huku anakula. Isitoshe akikwamwa na chakula au kufikwa na kitu, hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (32) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-10-17.mp3
  • Imechapishwa: 15/11/2014