Kula kwa kutumia mkono wa kushoto

Swali: Ni ipi hukumu ya siku zote mtu kula au kunywa kwa kutumia mkono wa kushoto? Baadhi yao wanaona kuwa ni jambo lililochukizwa.

Jibu: Si kwamba ni baadhi yao. Wanachuoni wote wanaona kuwa ni jambo limechukizwa. Hawaoni kuwa ni haramu kwa sababu haya ni katika mambo ya adabu. Sio katika hukumu ambazo zimesifika uharamu au uhalali. Hizi ni katika adabu za Kishari´ah. Kula na kunywa kwa kutumia mkono wa kushoto imechukizwa. Mtu kudumu katika jambo lililochukizwa linaweza kugeuka kuwa haramu. Kwa sababu ni dalili kuwa mtu hajali.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam (09) http://ajurry.com/safrawy/chorohat-elakida/chorohat-nawakid-elislam/charh-salah-fawzan/09.mp3
  • Imechapishwa: 07/04/2019