Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema katika Hadiyth Swahiyh:

“Usiku ukija hapa – yaani maghrib – na ukande wake zake mchana hapa – yaani mashariki –  na jua likatua basi atakuwa amefungua mwenye kufunga.”

Au maneno mfano wa hayo aliyosema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Imetubainikia baada ya upelelezi ya kwamba jua linazama kikweli kabisa kiasi cha takriban dakika tano au saba baada ya muadhini kuadhini hapa Kuwait. Je, inajuzu kuadhini kabla ya muadhini lakini baada ya kuhakikisha kuwa jua limeshazama?

Jibu: Mfungaji akihakikisha kuwa jua limeshazama na magharibi imeshaingia basi imehalalika kwake kula. Amesema (Ta´ala):

ثُمَّ أَتِمُّوا الصِّيَامَ إِلَى اللَّيْلِ

“Kisha timizeni swawm mpaka usiku.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Usiku ukija hapa na ukande wake zake mchana hapa na jua likatua basi atakuwa amefungua mwenye kufunga.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

Kwa haya inapata kutambulika kuwa zile jadwali za swalah zinazoenda kinyume hazitakiwi kutiliwa maanani. Vilevile haikushurutishwa kusikia adhaana baada ya kuhakikisha kuwa jua limeshazama.

[1] 02:187

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/287)
  • Imechapishwa: 14/06/2017