Swali: Muislamu akiendelea kula wakati wa daku mpaka kukachomoza alfajiri na hajui kama ajizuie na chakula ambapo akaendelea kufunga siku hiyo. Je, ana swawm au anawajibika kulipa?

Jibu: Wajibu kwa muislamu ambaye anafunga swawm ya faradhi ajizuie na kula pale ambapo alfajiri inachomoza. Akila au kunywa baada ya kuchomoza alfajiri basi swawm yake inaharibika na itakuwa ni wajibu kuilipa siku hiyo. Allaah (Subhaanah) amesema:

وَاشْرَبُوا حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ ۖ ثُمَّ أَتِمُّوا الصِّيَامَ إِلَى اللَّيْلِ

“Kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu uzi mweupe wa alfajiri kutokana na uzi mweusi. Halafu timizeni swawm mpaka usiku kisha timizeni swawm mpaka usiku.” (02:187)

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/183)
  • Imechapishwa: 29/05/2018