Kukusudia kuchukua likizo wakati wa sikukuu za kikafiri kama krismasi

Swali: Kumetokea kati yangu mimi na ndugu zangu waislamu mjadala kuhusu dini ya Uislamu. Baadhi ya waislamu Ghana wanatukuza likizo za kiyahudi na wakristo na wanaziacha likizo zao kiasi cha kwamba zinapofika sikukuu za mayahudi na wakristo wanafanya masomo ya Kiislamu kuwa na likizo kwa sababu ya mnasaba wa sikukuu zao na zinapofika sikukuu za waislamu hawayafanyi masomo ya Kiislamu kuwa na likizo na wanasema kwamba eti wakifuata likizo za mayahudi na waislamu wataingia katika dini ya Uislamu. Ee Shaykh wetu! Tunaomba utufahamishe matendo yao ni sahihi katika dini?

Jibu: Kitu cha kwanza Sunnah ni kudhihirisha nembo za kidini za Uislamu kati ya waislamu na kuacha kudhihirisha za kwao kwa sababu ya kwenda kinyume na mwongozo wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Imethibiti kutoka kwake kwamba amesema:

“Jilazimieni na Sunnah zangu na Sunnah za makhaliyfah waongofu. Shikamaneni nazo barabara na ziumeni kwa magego… “

Kitu cha pili haijuzu kwa muislamu kushirikiana na makafiri katika sikukuu zao na kudhihirisha furaha juu ya mnasaba huu na akaacha kazi. Ni mamoja kazi hiyo ni ya kidini au ya kidunia. Kwa sababu kufanya hivo ni katika kushirikiana na maadui wa Allaah, kitendo ambacho ni haramu, vilevile ni katika kusaidiana pamoja nao juu ya batili. Imethibiti kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba amesema:

“Mwenye kujifananisha na watu basi yeye ni katika wao.”

Allaah (Subhaanah) ameesema:

وتعاونوا على البر والتقوى ولا تعاونوا على الإثم والعدوان واتقوا الله شديد العقاب

“Saidizaneni katika wema na kumcha Allaah na wala msisaidizane katika dhambi na uadui. Mcheni Allaah. Kwani hakika Allaah ni mkali wa adhabu.” (05:02)

Nakunasihi kurudi katika kitabu “Iqtidhwaa´-us-Swiraatah al-Mustaqiym” cha Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah). Hakika ni chenye faida sana katika maudhui haya.

Raisi: ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

Naibu wa raisi: ´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

Mjumbe: ´Abdullaah bin Qu´uud.

Mjumbe: ´Abdullaah bin Ghudayyaan.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.ajurry.com/vb/showthread.php?t=2988
  • Imechapishwa: 19/12/2019