Swali 224: Je, swalah zikusanywe ilihali mtu yuko nyumbani kwake?

Jibu: Aswali kila swalah ndani ya wakati wake. Haijuzu kwake kukusanya. Anatumia dalili Hadiyth ya Ibn ´Abbaas kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikusanya al-Madiynah pasi na kuwa na khofu wala mvua. Iwapo mtu atakusanya katika maisha yake mara moja, mara mbili, mara tatu au mara nne [ni sawa]. Ama kuendelea katika hali hiyo, kama wanavofanya waliopatwa na huzuni, haifai.

Ama kukusanya wakati wa mvua ipo Hadiyth dhaifu ambayo ni Mursal. Kwa sababu Mursal ni miongoni mwa aina ya Hadiyth dhaifu. Inasema kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikusanya siku kuliponyesha mvua. Inafaa kwake kukusanya wakati kunaponyesha mvua. Lakini asifanye ndio mazowea. Hayo ni kutokana na dalili inayoonyesha kwamba inafaa kwake kuswali nyumbani kwake. Hadiyth inasema:

“Swalini majumbani mwenu.”

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ijaabatu as-Saa-il, uk. 440-441
  • Imechapishwa: 28/10/2019