Kukusanya picha kwenye kitu kwa sababu ya kumbukumbu


Swali: Inajuzu kukusanya picha kwa ajili ya kumbukumbu?

Jibu: Haijuzu kwa muislamu yeyote, mwanaume na mwanamke, kukusanya picha kwa ajili ya kumbukumbu. Namaanisha picha za viumbe wenye roho. Ni mamoja kiumbe huyo ni mwanaadamu au kitu kingine. Bali ni wajibu kuzichana. Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba alisema kumwambia ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh):

“Usiache picha isipokuwa umeiharibu wala kaburi lililoinuliwa isipokuwa umelisawazisha.”[1]

Vilevile imethibiti ya kwmaba (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza mapicha majumbani.

Isitoshe pindi (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipoingia Ka´bah siku ya kufunguliwa mji wa Makkah aliona kwenye ukuta wake picha akaomba maji na kinguo kisha akaifuta. Kuhusu picha za viumbe visivyokuwa na uhai, kama vile mlima, mti na kadhalika hazina neno.

[1] Muslim (969), at-Tirmidhiy (1049), an-Nasaa´iy (2031), Abu Daawuud (3218) na Ahmad (01/96).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (04/225)
  • Imechapishwa: 16/07/2017