Kukusanya mtu akiwa nyumbani kwa kuchelea gari haitosimama njiani

Swali: Nikinuia safari na nikaswali Dhuhr mjini kwangu inafaa kwangu kutanguliza ´Aswr nikaikusanya pamoja na Dhuhr nikichelea kupitwa na swalah ya ´Aswr khaswa kwa kuzingatia kwamba gari sio miliki yangu na pengine isisimame njiani isipokuwa baada ya jua kuzama. Au inafaa kuswali hali ya kukaa ndani ya gari na huku gari inaendelea na safari?

Jibu: Hakuna neno kukusanya katika hali hii. Kwa sababu kukusanya ni ruhusa. Kila ambapo mtu anahitajia kukusanya basi anaweza kufanya hivo. Kwa ajili hii imethibiti katika “as-Swahiyh” kupitia kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikusanya al-Madiynah pasi na khofu wala mvua. Alipoulizwa makusudio yake ya kufanya hivo akajibu: “Alitaka asiwatie uzito Ummah wake kwa kuswali kila swalah ndani ya wakati wake”. Ukijua kuwa gari hii sio milki yako na huenda haitosimama ikianza safari baada ya Dhuhr isipokuwa baada ya jua kuzama, basi inafaa kwako kukusanya Dhuhr na ´Aswr ukiwa bado uko nyumbani kwako. Lakini katika hali kama hii unatakiwa kuziswali Rak´ah nnenne na si Rak´ah mbilimbili. Kwa sababu bado hujaanza safari.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (09) http://binothaimeen.net/content/6721
  • Imechapishwa: 30/11/2020