Swali: Je, katika mfumo wa Salaf ni kukusanya makosa ya mtu fulani na kuyaanika kwenye kitabu ili watu wayasome[1]?

Jibu: Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu. Haya yanasemwa na wapotevu ili waweze kutetea Bid´ah zao, vitabu vyao, mifumo yao na watu wao watukufu.

Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wametaja mengi katika upotevu wao. Wamekusanya maneno ya mayahudi na manaswara na wakayakosoa katika Aayah za Qur-aan. Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah tangu hapo kale katika historia mpaka hii leo wamemzungumzia Jahm bin Swafwaan, Bishr bin Marriysiy na wakadhibiti Bid´ah na  upotevu wao. Vilevile wamekusanya maneno ya vipote na wakayakosoa. Ni nani anayeharamisha haya? Haya ni mambo ya wajibu.

Ikiwa watu watapotea kwa Bid´ah zao nyingi ambapo mtu akayakusanya sehemu moja na akayatahadharisha kwa majina yao, Allaah akujaze kheri. Kwa kufanya hivo basi utakuwa umesaidia kheri kubwa juu ya Uislamu na waislamu.

[1] Tazama https://www.youtube.com/watch?v=xucNCtBweCQ

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kanda: al-Ajwibah ´alaa As-ilah Abiy Rawaahah al-Manhajiyyah http://rabee.net/ar/questions.php?cat=26&id=603
  • Imechapishwa: 13/03/2018