Kukumbuka soksi ilikuwa najisi baada ya swalah


Swali: Kuna mtu amepangusa juu ya soksi yake na akaswali nazo, kisha akakumbuka kuwa soksi hizi ni najisi. Je, swalah yake ni sahihi?

Jibu: Swalah yake ni sahihi. Hata akiswali kwenye nguo najisi kwa kusahau najisi hiyo au hakujua kuwa ina najisi isipokuwa baada ya kuswali, swalah yake ni sahihi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (61) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13585
  • Imechapishwa: 16/11/2014