Swali: Yule anayemkufurisha ambaye ametumbukia katika moja ya mambo yanayovunja Uislamu anahesabiwa kuwa ni Takfiyriyyah?

Jibu: Kukufurisha kwa haki, huyu hawi Takfiyriy. Akimkufurisha yule ambaye anastahiki kukufurishwa, hii ni haki.

“Yule asiyemkufurisha kafiri, basi ni kafiri.”

Hili ni miongoni mwa yanayovunja Uislamu:

“Yule asiyemkufurisha kafiri, basi ni kafiri.”

Ama kukufurisha pasina haki, hili ndio limekatazwa. Huyu ndiye Takfiyriy. Yule ambaye anawakufurisha watu bila ya haki.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Fathul%2027-3-1435.mp3
  • Imechapishwa: 06/10/2020