Kukubaliana juu ya kupandisha bei

Swali: Ni ipi hukumu kwa wafanyabiashara kupatana kuuza bidhaa fulani kwa bei fulani?

Jibu: Maafikiano haya hayajuzu. Mtume (Swalla Allahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Waacheni watu waruzukiane wao kwa wao.”

Haijuzu kukubaliana juu ya kupandisha bei. Bali hata serikali haijuzu kufanya hivo isipokuwa katika baadhi ya hali. Imekuja katika Hadiyth Swahiyh ya kwamba Maswahabah wamesema:

“Ee Mtume wa Allaah! Tuamulie bei fulani.” Ndipo akasema (Swalla Allahu ´alayhi wa sallam): “Allaah ndiye mwenye kuamua.”

Kusemwe nini ikiwa watu watakubaliana juu ya kupandisha bei kwa ajili ya kuwatumia watu?

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Raabigh (02)
  • Imechapishwa: 16/09/2017